Classmate Ama Sponsor? Mnataka Nicheke Nikiwa Wapi?
.jpeg)
Kimani Maruge, ndiye ako na history ya kuwa classmate mzee zaidi dunia nzima. Picha kwa hisani ya BBC. Knock knock… ladies, gentlemen, na wale wengine tunawapenda pia. By now najua mna hamu ya kuskia story ingine kutoka kwangu. Na kama kawaida, mimi sitawanyima. So hapa iko. Sasa, mimi si Genz bana… si hata karibu. Mimi ni focused millennial, lakini niko na appetite ya Gen Z (ukipata joke umepata, ukikosa... si vibaya kuuliza). Ni kama nimekua nikitoroka age yangu. Uso yangu iko na passport ya 20s, lakini kwa roho najua nimeshaingia third floor. Sasa siku moja, kwenye maadventures zangu za kawaida hapa Makutano (najua mnaijua), nikapatana na mtu. Alinipa reality check kali hadi nikaanza kujiuliza kama ni time nichukue life serious. But again, sitaki kueleza sana. I’m an adult… ama mimi si? Sasa niko joint flani ya mtaa, pale social spot, najichochat na wale wamevuta mbili tatu. Kama kawaida, mimi na-drop knowledge tu – unajua vile nawasha akili kwa watu already wasted. Halafu ghafla bi...